SITAKI

Sitaki kuna nikune, mi sina pangu kwenyewe?
Sitaki shika nishike, hayawi chanda na pete?
Sitaki nipe nikupe, mkononi kipi ‘rambwe?
Sitaki vuta ‘kuvute, shari na shani nipite?

Sitaki panda nipande, si cheo wala mziwe,
Sitaki rusha niruke, shazi, shamla na shangwe,
Sitaki tega nitege, sinayo maguru nne,
Sitaki vuta ‘kuvute”, shari na shani nipite?

Sitaki ufe nifiwe, moyo tena na udume,
Sitaki ule nisile, miwa, sato, nyama, kole,
Sitaki uje nijiwe, masikani cha udimbwe,
Sitaki vuta ‘kuvute, shari na shani nipite?

Sitaki koma ukome, urudi nyuma usome,
Sitaki zoma uzome, tumia ndimi tuseme,
Sitaki hema uheme, tuongee sisi dume,
Sitaki vuta ‘kuvute, shari na shani nipite?

Mroho Sinini 2023-11-20

 

ynshen