{"id":2358,"date":"2021-01-12T16:17:13","date_gmt":"2021-01-12T15:17:13","guid":{"rendered":"http:\/\/yellingstone.info\/?p=2358"},"modified":"2021-01-13T00:00:36","modified_gmt":"2021-01-12T23:00:36","slug":"fulltext-hotuba-ya-rais-john-magufuli-20210108-baada-ya-utiliaji-saini-wa-ujenzi-wa-reli-ya-sgr-mwanza-isaka","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/yellingstone.info\/?p=2358","title":{"rendered":"[FULLTEXT] Hotuba Ya Rais John Magufuli 2021\/01\/08 Baada Ya Utiliaji Saini Wa Ujenzi Wa Reli Ya SGR Mwanza-Isaka"},"content":{"rendered":"<p>HOTUBA YA RAIS JOHN MAGUFULI BAADA YA UTILIAJI SAINI WA UJENZI WA RELI YA SGR MWANZA &#8211; ISAKA<\/p>\n<p>2021\/01\/08 Chato<\/p>\n<p>Jamani, habari za asubuhi?<br \/>\nMheshimiwa waziri Wang Yi,<br \/>\nWaziri wa mambo ya nje kutoka China,<br \/>\nmheshimiwa profesa Kabudi, waziri wa mambo ya nje kutoka Tanzania,<br \/>\nWaheshimiwa mawaziri wote mlioko kwa upande wa Tanzania<br \/>\nna mawaziri upande wa China<br \/>\nmakatibu wakuu, watendaji mbalimbali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,<br \/>\nna wakuu wa taasisi mbalimbali mlioko hapa, nami&#8230;<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNami napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza<br \/>\nkampuni ya Kichina iliyoshinda tenda ya kujenga kilomita 341<br \/>\nza ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka<br \/>\nNa mimi nina matumaini kwamba watafanya kazi kwa uadilifu mkubwa<!--more--><br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nMheshimiwa waziri wa mambo ya nje kutoka China alileta ujumbe<br \/>\nkutoka kwa rais Xi Jinping wa China kutuletea sisi Watanzania.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa hii ni kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China<br \/>\nya tangu mwaka wa 1964, 1965 wakati waasisi wa mataifa haya<br \/>\nMwl. Nyerere pamoja na Mao Zedong walivyoweka maelewano mazuri<br \/>\nna kuwezesha uhusiano huu wa nchi mbili kuendelea kikamilifu hadi leo.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nUjumbe wa kutoka rais wa China, nimeupokea.<br \/>\nLakini na mimi nimetuma ujumbe mwengine kule amfikishie mheshimiwa rais wa China.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa mimi katika makubwa uliyomueleza ni kuhusu kuendelea kushirikiana katika nchi hizi mbili katika maswala ya kiuchumi.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNimemuomba watusaidie katika miradi mitatu mikubwa ambapo ni ujenzi wa hydroelectric power kule Njombe, Lumakari, pamoja na Luhuji, majina ya Kihehe.<br \/>\nLakini pia nimemuomba watujengee kilometa 148 kule Zanzibar za Highway.<br \/>\nNa hili amelisema wanakwenda kulishughulikia na atafikisha ujumbe kule.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nLakini pia nimemuomba wakatusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa.<br \/>\nMoja ya deni ambalo tunadaiwa ni milioni 15.7, za deni tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA.<br \/>\nLakini kuna deni pia la nyumba za maaskari wetu ambao wamekuwa wapiganaji wazuri<br \/>\nna wameshiriki katika misheni mbalimbali za kimataifa ambalo<br \/>\nnyumba zile zinahusu karibu dola milioni 137 na tumeshalipa zaidi ya dola milioni 164<br \/>\nLakini deni lingine ni la Urafiki, kiwanda cha Urafiki, dola milioni 15.<br \/>\nHaya nayo nimemuomba wakatufutie tu kwa sababu nchi ya China ni rafiki yetu lakini pia ni nchi tajiri.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa mheshimiwa waziri amesema atalifikisha hili ombi China.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nIli waangalie namna ya kuweza kutusamehe na hasa katika ma-sheria zao za concessioning huwa ni kazi kubwa kusamehe madeni lakini wamesema watalifikisha kule.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nLakini nilimueleza urafiki wetu wa kati China na Tanzania ni mkubwa sana ndiyo maana leo tumeshuhudia utiaji wa saini hapa wa gharama ya dola za marekani bilioni [sahihi: trilioni] 1.32 ambao ni sawa na trilioni 3.026.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa uhusiano huu umekuwa siku nyingi na ndiyo maana mheshimiwa waziri ameeleza hapa kwa miaka kumi iliyopita makampuni yaliyofanya kazi za ujenzi katika nchi hii yamechukua fedha trilioni 21, sawa na dola bilioni 10.<br \/>\nNa zimelipwa na walipakodi Watanzania. Huu ndio uhusiano na huu ndio undugu.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nKwa hiyo nina uhakika hata yale maombi yangu yatasikilizwa vizuri kwa sababu makandarasi wameshachukua trilioni 21 katika siku 10 tu, katika miaka kumi tu.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nLakini kubwa lingine ambalo tumezungumza tumeeleza uhali halisia kwamba China ni nchi tajiri humu duniani.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa sisi Tanzania tuna mazao mengi ambayo tunaweza tukayapeleka China.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa ndiyo maana katika zawadi zangu nimetoa korosho,<br \/>\nnimetoa majani ya chai, nimetoa kahawa nikiamini kuwa<br \/>\nsisi Tanzania tuko milioni 60, Wachina wako bilioni 1.4 hadi 5, wakila tu nusu kilo ya korosho zetu maana yake watakuwa wanakula tani milioni 750. Korosho zote za Tanzania zitakuwa zimeisha nafikiri hata za Afrika nzima.<br \/>\nKwa hiyo iwe kitambulishwe kwamba wakaanze kula korosho za Tanzania badala ya kununua korosho sehemu nyingine.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nKwa hiyo nitoe wito kwa Watanzania wenzangu huu ndio wakati wa kulishika soko la China, kwa sababu, idadi ya Wachina iliyoko katika dunia ambao ni bilioni 1.5 inazidi idadi ya waafrika wote katika Afrika ambao tuko bilioni 1.2.<br \/>\nSisi tuko milioni 60. Mazao yetu tuwe tunapeleka kule. Kama ni pamba, tupeleke kule, kama ni kahawa, wote wakanywa kijiko kimoja kimoja ukizidisha vijiko bilioni 1.5 utajua utakuwa umeuza kilo ngapi.<br \/>\nTupeleke mihogo yetu, tupeleke samaki wetu, tupeleke mazao yetu<br \/>\nna hasa mazao ambayo tume-add value.<br \/>\nNina uhakika kwa kutumia Wachina, uchumi wa Tanzania utapanda sana sana.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nNa hii ndiyo faida ya kuwa na watu wengi.<br \/>\nNa mimi mimemuhakikishia kufanya biashara na Tanzania atakuwa amefanya biashara na Afrika Mashariki ambapo tuko watu milioni 165.<br \/>\nLakini atakuwa direct amefanya biashara na SADAC ambako tuko zaidi ya watu milioni 400 hadi 500.<br \/>\nKwa hiyo karibu zaidi ya watu milioni 500 atakuwa anafanya nao biashara kwa kufanya biashara na Tanzania, kwa sababu sisi ni wanachama wa nchi hizo.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nKwa ujumla, taarifa tuliyoletewa na mazungumzo tuliyoyafanya yalikuwa mazuri.<br \/>\nNa nimemuhakikishia kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu China ni ndugu zetu.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nBaada ya kusema haya niwatakie mafanikio mema, niwashukuru sana waliofuatana na mgeni wetu ndugu Wang Yi pamoja na ubalozi na wengine wote waliokuja.<br \/>\nLakini niwashukuru sana mawaziri na watendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wa kiongozi wana mheshimiwa Profesa Kabudi kwa mazungumzo mazuri waliyoyafanya.<br \/>\nNa nina uhakika wamefikia muafaka wa mambo yote.<br \/>\nSasa ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote na kuonyesha ushirikiano mkubwa sana.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nMheshimiwa waziri, karibu sana. Ndugu walikwa wote karibuni sana. Xiexie.<br \/>\nNafikiri chakula kitakuwa kiko tayari, twendeni tukale chakula ili kusudi tuendelee na mambo mengine.<br \/>\nNinawashukuru sana pia kwa kuja hapa Chato.<br \/>\nLakini nitoe wito kwa kontrakta ahakikishe hiki kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka kinafanywa kwa haraka zaidi, lakini pia niwaombe kama ombi lilivyotolewa na mheshimiwa waziri kwa serikali ya China.<br \/>\nKatika kipande hilichobaki cha Isaka hadi Makutupora.<br \/>\nkama wataweza hata kutukopesha kwa Concession,<br \/>\nsisi tutafurahi sana ili kipande kinacho kiweze kujengwa kwa sababu kitasaidia sana katika kujenga uchumi wa nchi yetu.<br \/>\nNa baadaye tutaendelea na Tabora hadi Kigoma na maeneo mengine.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nChina oyee<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nXi Jinping oyee<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nTanzania oyee<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nWang Yi oyee<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nAhsanteni sana ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.<br \/>\nNinampongeza sana mheshimiwa Wang Yi anajua Tanzania hatuna Corona.<br \/>\nNdiyo maana hakuvaa hata yale mabarakoa.<br \/>\nAhsante sana mheshimiwa Wang Yi.<br \/>\n[ukalimani]<br \/>\nAhsante sana nashukuru sana na mimi kwa kumthibitishia nakwenda kumshika mkono twende tukale chakula pamoja.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HOTUBA YA RAIS JOHN MAGUFULI BAADA YA UTILIAJI SAINI WA UJENZI WA RELI YA SGR MWANZA &#8211; ISAKA 2021\/01\/08 Chato Jamani, habari za asubuhi? Mheshimiwa waziri Wang Yi, Waziri wa mambo ya nje kutoka China, mheshimiwa profesa Kabudi, waziri wa mambo ya nje kutoka Tanzania, Waheshimiwa mawaziri wote mlioko kwa upande wa Tanzania na mawaziri <a class=\"read-more\" href=\"http:\/\/yellingstone.info\/?p=2358\">&hellip;&nbsp;<span class=\"meta-nav\">&rarr;<\/span><\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":[],"categories":[1],"tags":[],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2358"}],"collection":[{"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=2358"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2358\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=2358"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=2358"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/yellingstone.info\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=2358"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}