Uhuru关于BBI的演讲全文

2019年11月27日,在内罗毕的Bomas of Kenya,肯尼亚几乎所有的政治家都出席了关于BBI的发布会。总统Uhuru的演讲时最近几年听到的最有力的一次演说。

链接:https://www.youtube.com/watch?v=EAPOkblKFfY

Ahsanteni wenzangu tuketi nashukuru
wenzengu hamjambo
hamjambo tena
(hatujambo)
ebu tusalimiane tu tafadhali hata wale wako nje
tusalimiane sote
kama wakenya ambao wamesanyana hapa Bomas of Kenya
siyo kwa sababu ya mtu
lakini kwa sababu yetu sisi wote
kaimu wa rais, mheshimiwa Raila Amolo Odinga
viongozi vya vyama mbalimbali za kisiasa
waheshimiwa wabunge
maseneta, magavana, ma-MCA
viongozi wa kidini, viongozi wa akina mama
wenzetu mabalozi ambao wamehudhuria leo
na haswa mgeni wangu wa kipekee siku ya leo
waziri wa nchi za nje wa Tanzania
ndugu Kabudi ambaye mimi namwita „Kafudhi“

wakenya wenzangu,
siku ya leo ni simu muhimu
na vile nimesema, siyo siku muhimu kwangu mimi
lakini ni siku muhimu kwa wananchi milioni 47 wakenya wazalendo ambao
twajua katika kila kona ya taifa letu la Kenya leo
wanaangalia runinga, wengine wako kwa maredio
na wote, macho yao, fikra zao,
ziko pamoja nasi katika kongamano hii hapa Bomas
na ni kwa nini?
Ni kwa sababu
kila mkenya pahali popote alipo, anataka kusikia
mambo yale ambayo yanajadiliwa hapa Bomas
ambao tunaanzisha kujadili kama wakenya hapa Bomas of Kenya.
Itabadilisha maisha yao ya kikawaida kwa njia gani?
Nimeshukuru wale wote wote wote wote
ambao wameongea siku ya leo
kwa maono yao na kwa kuunga mkono ya kwamba yastahili wakenya wazalendo wawe [na] nafasi
wawe [na] nafasi ya kuongea pamoja
kuhusu taabu mbalimbali, shida mbalimbali,
ambazo zinakumba maisha yao
na nikiwashukuru wote ambao wameongea
ningependa sana kumshukuru, ndugu Kabudi,
kwa sababu yeye ndiyo ameongea roho yangu.
Wenzetu, kwa muda mrefu,
tumeamua – na sijui ni kwa nini –
tumeamua kama wakenya ya kwamba
njia ya kujadiliana pamoja ni kusimama kwa jukwa na kutoa maneno
sana sana na hata bila mtu kufikiria
kwa sababu nataka nipigiwe makofi
tunaelewana? Na ndipo tunaona sana sana
ajenda ya taifa inakwama
kwa sababu ukisimama kuongea kama kiongozi
wewe unajiangalia kwanza wewe mwenyewe
ni nini nitafanya aidha nipigiwe makofi
ama nipigiwe kura
ama niseme kitu ingine ambayo itasaidia ule mtu karibu na mimi apigiwe kura,
so kama mambo ya ukabila, twasema
sisi wakikuyu tusema “Twaire ma mûciî (Tuongee maneno ya nyumbani)”
wengine wanasema tuongee yetu hiyo msiongee sana watu wasisikie lakini unajua yule ndio wetu yule.
my friends,
tumekosa kuongea kama jamii moja ya baba na mama wazalendo wa Kenya.
siku ya leo tuko hapa
kwa sababu – na ni vizuri kurudi nyuma si kweli –
kwa sababu baada ya uchaguzi wa 2017 kulitokea matatizo
na kwa ukweli kama rais mimi ningesema nimeshinda
na nitatawala, na hakuna mtu angenizuia jameni kwa sababu ukila kiapo, tosha gari, twende mbele
na hiyo ndiyo ukweli,
kwa lakini, taifa hii letu lilikuwa na mgawanyiko katikati
kuna sehemu zingine tuseme mji wetu mjuu wa Nairobi
ukiwa kabila hili, ukikanyanga au ukiingia, ni mawe
mnajua watu wanasahau ukiingia upande mwingine, ni taabu.
kiosk yako inachomwa,
mama mboga zake zakanyangwa
jameni, dunia yetu ilikuwa imejaa hofu
ukitembea barabara kwanza lazima ujipange
utapitia wapi ehee ehee ehee
ati ndio ufike pahali ambapo ulikuwa unaenda
these are the truths
kwingine, watu wanasema
huyu ni rais, huyu mwingine mimi sijui huyu
ni namna hii ni namna hii
wafanyibiashara ndio hofu
hakuna mtu anataka kuendelesha biashara zake
kwa sababu unajiuliza: “kesho tutakuwa namna gani?”
na ndipo tukaonelea.
jameni, that is not a life.
hatukuchaguliwa kwa sababu yetu sisi,
tulichaguliwa kwa sababu ya maslahi ya wale sasa wamejazwa na hofu maishani mwao
na ni jukumu letu kama viongozi tuje pamoja
siku ya leo, na nimesema hapo awali tena,
nataka kumshukuru ndugu yangu mheshimiwa Raila Odinga
kwa sababu, kukutana kwetu mara ya kwanza, he, haikuwa kitu rahisi
kila mtu pia, hiyo hofu mlikuwa naye, hata sisi tulikuwa naye pia
huyu mtu, tulikutana naye tutaambiana nini?
tutasema nini?
na kwa ukweli wakati tulikutana tulikunywa chai karibu dakika 45 hakuna mtu anaongea
tunakunywa tu chai – ehee
“habari za nyumbani” “sawa” ehee
“habari ya mama” “haa, ako tu” ehee
“habari ya watoto” “haya, wanasoma, wanaendelea” ehee hee hee
hakuna hakuna hakuna maneno ingine yanaweza kutoka, eh?
kwa sababu ya hasira ya yale ambaye tulikuwa tunarushania huko mbele
baada ya saa moja hivi sasa jameni ndipo sasa watu kuangaliana hapa tumejifungia ni sisi wawili tu
ndio mambo ikaanza karibu tulale huko sasa
na tukasema kitu kimoja wakati tulimaliza
tukasema, tofauti zetu siyo kubwa vile
mashindano ndiyo inatuletea shida hii yote
kwa sababu fikra siyo tofauti
na ndipo tukasema jameni wacha tuketi hata tuwache uchaguzi huu wa 2017
wacha turudi nyuma, ni kwa nini baada ya kila miaka mitano
wananchi wa Kenya lazima wapigane
lazima tumwage damu
lazima mali iharibiwe
lazima biashara zisimame
lazima hofu iingie wa wakenya
na tukasema turudiiii nyumaaa na tujiulize
huu ndio ulikuwa mwanzo wa BBI
na tukasema, huu uchaguzi wa 2017 sio wa mbele, na sio wa mwisho
bado utakuwa na uchaguzi mwingine kwa sababu
Kenya ni nchi democratic
Kenya ni nchi ambaye tuna demokrasia
bado itakuwa na uchaguzi
kwa hivyo jambo muhimu yetu sisi kama viongozi
ni kwanza tuwache kofia zetu za kisiasa
tuwache kofia zetu za vyama vyetu
na tujiulize ni nini inasababisha tupigane
na ndio turekebishe mambo haya
tuweze kuhakikisha ya kwamba
kwa sababu uchaguzi bado utakuja
ya kwamba tutaweza kufanya uchaguzi katika taifa letu la Kenya bila umwagikaji wa damu
bila uharibifu wa mali,
bila hofu kwa wananchi
na hiyo ikawa lengo letu kubwa
sasa, taabu unajua siasa
ukishikana na mwazako, mwingine anasema hawa wana… wanapanga nini?
hee? ndio wanaambia hii sisi wanasiasa ndio chafu ya nchi hii
wanapanga nini?
sasa unaona?
mwingine sasa hee wale sasa wako na njama.
na Kiraitu mwenyewe amesema hapa sijui kama anajua vile alikuwa anasema hee?
unaona wale wali… hata sisi wacha sisi tukutane na sisi tujipange, sisi tuwe na story yetu
na wengi wakasahau na ningependa leo kuwakumbusha wenzangu wakenya
ya kwamba vita ya 2017 na au shida ya 2017 siyo ya kwanza
wenzetu 20… ehm… 1992 tulipigana
wenzetu 1997 tulipigana
wenzetu 2002 muungwana ambaye anaitwa Uhuru Kenyatta
hata mbele kura kuisha
akasema nimekubali nimeshindwa tukawa na amani
tukumbuke tukumbuke
kwa sababu tunasahau
na ambaye anasahau hajui tena anarudia makosa
tukuje 2007 tukapigana
jameni tukapigana mpaka mimi mww…
kwanza mimi nimekuwa nimepelekwa kwa wazungu
huko kwa sababu ilikuwa inasemekana kwamba
huyu ni mtu ambaye anataka kufungiwa huko…
anyway, hiyo ni story ingine.
na sana sana wengine wakasahau pia ya kwamba 2010
nikaenda nikatafuta ndugu yangu pia William Ruto
heya, nikawambia sasa jameni hii na watu wetu wanaumia.
nikaenda nikamshika mkono, akanishika mkono
tukasema hatuwezi kuendelea namna hii
na tukawa na amani
na hiyo hiyo ndiyo nia yangu na ndugu yangu mheshimiwa Raila Amolo Odinga
tushikane mkono, ndiyo tuwe na amani
lakini taabu ya siasa, wenzangu ni ya kwamba
ukishika huyu, yule mwingine anakusema ni adui
ukishika huyu sasa, yule mwingine ni adui
ach, let us now be mature, ya?
let us now be mature.
And I appeal especially to the political class.
don’t divide these people, they don’t deserve it.
we are here talking about maslahi yao.
we are here talking about their peace
and once we assure them and we give them an enabling environment,
these 47 million people are mature enough to elect the leaders that they want
ours is to enable them to do so
and to respect their wishes
this is not a time
this one versus that one
there will come that time
na hawa na wale wengine wanatuangalia kwa runinga
na wale ambao wanasikiza kwa redio
na wale ambao wako kwa maofisi zao
na wale ambao wako mashambani
siku ikifika, wakenya sio wajinga, wataamua
yetu sisi si kuja kuleta mgawanyiko kati yao
wacha tuwatengenezee shida zao
tutengeneze shida za kisiasa
kwa sababu kwa ukweli taabu moja katika siasa zetu ni kwamba
tukiingia mashindano
wale ambao wanashinda, tunasema tumeshinda
wale ambao wameshindwa, wanasema sasa sisi tuko wapi
hiyo ndiyo kitu inaleta shida
so, lazima tutafute system sisi kama wakenya
ya kuhakikisha ya kwamba kila mkenya atajisikia yeye ni mshindi
au ni namna gani mwenzangu
kila mkenya pahali alipo ajisikie yeye ni mshindi
tutengeneze hii nchi ya kwamba twaweza twende tupige kura
mtu anarudi nyumbani, anapumzika na watoto wake
anapumzika na ndugu zake
anangojea matokeo
akijua yeye pahali amepiga
lakini akijua pia yule amepigia akishindwa
anasema ach, tse tulijaribu lakini tumeshindwa
lakini kwa roho yake anajua ya kwamba
hata yule ambaye ameshinda
hatakuja kumnyang’anya shamba yake
hana uwezo ya kumkosesha kazi
hana uwezo ya kumnyima pesa zake na haki yake
hana uwezo ya kusimamisha madawa kwa hospitali yake
anasema nitangojea miaka ingine mitano tushindane tena hamna shida.
So that we differ on policies my friend
we don’t differ on who has won
ati huyu akishinda wale wengine wanasema
ahh huyo siyo rais wangu, eh?
huyo siyo mheshimiwa wangu
huyo siyo seneta wangu
huyo siyo gavana wangu
huyo ni wako
tunataka yule ambaye atashinda ni kiongozi wa wote
waliompigia na wale ambao hawakumpigia
turekebishe hiyo, jameni wenzangu
na hiyo siyo taabu
na hiyo siyo inataka
let us talk about it and find out
what it that that we can do to make sure
that the resultant, product of an election is inclusive and nobody feels left behind.
nobody feels left behind
kura ni siri, kura ni siri
kulingana na maono ya wananchi
na kulingana na maneno ya wale ambao wanatafuta kura
we shouldn’t force each other that we must accept
mimi ni mkikuyu lazima nimpigie mkikuyu
mimi ni mkalenjin aaahh huyo ndiyo mtu yangu
mimi ni mjaluo baba akisema tumesema, hapanaaa, hapanaa
siku ambaye tutajua tumeshinda
ni siku ambayo kama Raila anatafuta kiti
aende Kiambu na apewe kura kabisa
kama ni Ruto atafuta kiti
aende mpaka Siaya na apatiwe kwa sababu ya yale amesema
hay jameni
kuna story nimerudia na nitarudia leo
wengine wanakasirika nikisema, lakini siyo…
mi nasema kwa roho safi
kwa sababu hiyo ndiyo furaha yangu, unaona
kutoka tushikane mkono na baba, mi.. hey..
juzi tulikuwa na uchaguzi Kibera.
si ni kweli?
na mimi mnajua ndiyo kiongozi wa Jubilee,
na mimi nilikuwa na candidate
na tumesaidia candidate wetu kabisa,
si ni hivyo? ya?
sasa, kampeni ilikuwa moto, na zilikuwa zimechacha
hata nyinyi, mlikuwa mnajionea kila siku
hii hee, hii hee,
kampeni zilichacha, kweli ama siyo kweli?
eh demokrasia ilikuwa imewaka moto Kibera.
sasa mimi nasema, kweli kulikuwa vurugu kidogo kidogo
lakini ukiangalia ni viongozi walikuwa wanalimana na mawe,
hawa wanaweza kwenda Nairobi Hospital.
he?
mwananchi alikuwa anaruka mkutano hii, anaenda hii
sasa nimekuwa naambia wengine “usiku ya kuhesabu kura”
kuna mama mwingine rafiki yangu nilikuwa naongea na yeye ali… ni Campaigner wangu
sasa, nikampigia nikamuuliza “hali huko…?”
unajua sana sana hali huko wakati ya uchaguzi ilikuwa tension juu
nikamuuliza “hali iko namna gani? mko sawa?”
ah, akaniambia “sisi tuko sawa, lakini
hapa Kibera, ni kilio peke yake.”
nikamuuliza, “eh, kilio? kwani kuna shida gani?”
akaniambia, “ahh, jameni, Uhunye we.
mngeruhusu hii kampeni iendelee wiki ingine mbili.
jameni tukule mambo hapa mambo ilikuwa mingi huku.
(mcheko kwa muda mrefu)
kwa nini nyinyi mmefunga hii kamp…
tungeendelea wiki ingine mbili” eeh?
sasa, kesho yake kuchukua ripoti zile nachuanga asubuhi
nikaambiwa hee mambo Kibera namna gani?
nikaambiwa hee askari wale wote walikuwa wamesimamia uchaguzi wote wamerudi kwao
watu leo.. kila mtu ameelekea kwake kazi
mama ambaye alikuwa anatandika ndizi zake, ametandika
wa kupika samaki ameanza
harufu ya samaki sasa inasikika huko
mbeleni ilikuwa nyama kwa sababu pesa ilikuwa mingi
sasa ni samaki
(mcheko kwa muda)
hehe, hakuna kiosk ilikuwa imechomwa
hakuna mtu ambaye alikuwa hospitali
dunia ilikuwa imerudi
nikasema jameni
hata kama candidate wangu ameshindwa Kenya imeshinda
(makofi)
na hivyo jameni ndivyo twataka taifa letu liwe
hivyo ndivyo twataka taifa letu liwe
na hiyo ndiyo mimi nasema
yale ambao wametupatia wenzetu, wazee hawa wakiongozwa na mzee Yussuf Haji
mambo haya ndiyo tunataka tujadiliane pamoja
How can we maintain this peace?
How can we entreanch this peace?
How can we… na ndipo nasema kwa sababu siyo tu mambo ya kisiasa
tuangalie kindani ni nini inatukula
tukisema twataka maendeleo
ebu tuangalieni jameni
maendeleo na umaskini ni mwingi
maendeleo yako, umaskini ni mwingi
maendeleo iko, umaskini bado uko
so lazima tujiulize ni nini inakula
what is eating the other one?
na kitu kimoja mimi naweza nisema hapa, tuseme kwa ukweli
haswa tena tukiwa mji mkuu wa Nairobi
ukianglia dokument zote za serikali
zote za serikali zasema ya kwamba
mji ambao ndio tajiri ama jimbo ambalo ndiyo tajiri katika taifa la Kenya ni Nairobi
kweli ama siyo kweli?
ndiyo jimbo ambalo lina utajiri mwingi katika taifa letu la Kenya
na kwa hivyo hata kwa allocation ya ma-resources,
Nairobi inapata pesa kidogo sana
kulingana na umati wa wananchi ambao wanaishi katika huu mji.
lakini kuna kitu tumesahau sisi kama wakenya
hata kama huu utajiri uko hapa Nairobi
uko mikononi ya watu ngapi?
hiyo ni swali lazima tujiulize kweli ama siyo kweli?
huu mji ambao unasemekana ndio tajiri tuna wenzetu
ambao waamka kila siku kwenda kutafuta kibarua ya shilingi 150
kila siku, na hajui kama atapata, huyu ni tajiri?
kwa huu mji, tuko na wenzetu ambao hana maji… hawana maji safi ya kunywa.
katika huu mji, tuko na wenzetu ambao wanaenda choo kupitia makaratasi
mji tajiri
hii Nairobi, tuko na watoto ambao hawana nafasi katika mashule ya highschool
hata uniform watoto hawana
is this a rich county?
so we must look at that and ask ourselves
how are we using our resources?
and are our resources going to the people?
or are they going the leaders?
we must ask and adress ourselves, otherwise kwa ukweli tutamaliza hiyo umaskini Kenya hii?
tutakuwa tu tunasema tunaendelea
tuko na maendeleo lakini maendeleo hiyo haigusi kila mwananchi
again, that is what leads to… animousity, tension and anger because…
people feel they are excluded from the development that we are talking of.
sasa jameni hiyo kitu haina mambo ya kutusiana hapa na hapa
ni tukae tuseme this is the way we do
and I’m sure in every single county in this country
there are pockets that are wealthy and there are pockets that are very poor
how do we make sure that resources are matched to needs
how do we make sure …
that is the question surely we can discuss and talk about
that is nothing there to disagree about
wenzetu, fairer representation let us discuss it
so that we have an environment where everybody feels that they are represented by their respective leaders
and if we resolve this and many more things
like what is afflicting our young people
how can we create more jobs
nilisoma kidogo jana wakisema tuongeze pesa ambazo tunaweka katika ma-SMEs katika biashara dogodogo
kwa sababu hapo ndipo wananchi wengi wako
ndiyo tuweze kuinua hali ya uchumi it’s a good proposal friends
let us work on this together
hii nchi siyo nchi ya mashindano kati ya matajiri ati na maskini
hii ni nchi yetu sisi wote and we must come together
na ndipo nasema saa zingine wanasikia huyu anasema
oh wale wako namna hii
wale wako namna hii
wale wako namna hii
unajua sasa eh?
kwa sababu huyu rais ametoka hapo mali yote imeenda huko
kwa sababu rais ametoka… hakuna kitu kama hiyo.
rais ni rais wa wananchi milioni 47 na hiyo ndiyo inatakikana
na ndiyo twasema ikiwa ni bunge la taifa iwe ni bunge la kitaifa
tuache mambo ya maendeleo mashinani magavanas na ma-MCAs waende wafanye kazi ya mashinani, he!
I don’t think that is a problem.
na sisi tutengue masheria ni masheria gani ambaye inazuia wakenya kukua?
hiyo ndiyo kazi yetu hapa Nairobi.
hiyo ndiyo kazi yetu hapa Nairobi.
kule mashinani tuache wananchi wajue maji na mfereji inatakikana wapi
eeh, laini ya stima ni wapi ambaye inakosea
kabarabara gani… kanataka kutengenezwa huko
tunaelewana wenzangu?
tunataka kujiuliza ni kwa nini baada ya kila miaka mitano
tunaenda miaka mitatu ya kazi
miaka ya mbili tunapoteza kwa sababu siasa imechacha
tunataka tuulize wafanyibiashara wetu wenzetu ni nini inawazuia?
ni nini twaweza kufanya ndiyo tuhakikishe ya kwamba
biashara zenu hazisimami
hakuna taifa ambaye inaweza kuwa na mipangilio ya maendeleo ambaye itabadilisha maisha ya wananchi ikiwa mipangilio yetu ni ya miaka mitano.
lazima tuwe na mipangilio ya miaka ishirini.
haiwezi kuwa ati miaka mitano sasa tena hofu. hapana.
we must have development plans that are twenty years plus.
if we have to resolve our problems my brothers and sisters au ni namna gani wenzangu? eh?
na lazima tusema ya kwamba tunataka siasa ambazo zinatoa hizo hofu kwa wananchi
na ndio wafanyibiashara wetu waweze kupanga wakienda mbele.
tunataka hizo siasa ambazo zitawezesha
sasa siku hizi kwa Kenya huwezi kupata mkopo ndiyo nilikuwa naambia watu jana
wewe huwezi kupata mkopo wa zaidi ya miaka tano.
sana sana ni mkopo wa mwaka mmoja mwaka mmoja na … mbili
eh? sasa ni biashara gani itarudisha pesa na miaka mbili ama ni kweli ni biashara ambaye itakua.
lakini, mwenye kukopesha anasema “Aiyee, hii dunia hii mimi wache nipate yangu nitakopesha miaka miwili ningojee kwanza hiyo uchaguzi itakuwa namna gani.”
tunataka tuwapatie assurance ya kwamba wanaweza kupatia wananchi mikopo ya miaka kumi, ya miaka na tano
kwa sababu they have confidence ya kwamba Kenya will be stable and Kenya will have always leadership whoever it is
that will live within the rule of law
and that will respect their rights of all of our people
then we are moving forward
tunataka tuheshimiane kama makabila
ya kwamba kila mtu mkenya awe ako na uhuru wa kuwa pahali popote katika taifa hii letu la Kenya
na asisikie ya kwamba eh uchaguzi unakaribia
wacha sasa nipange virago ati nirudi kule nilizaliwa nitarudi tena uchaguzi ukiisha
we don’t want to live like that
we want to live in a manner in which we can program ourselves
na ndipo mimi nawauliza haswa nataka kurudia tena
viongiz wenzangu tafadhalini
ambition, ambition, personal ambition … is not bado
it’s a healthy thing
we all want to be ambitious because we are desirous
we want to power
we want to be MPs
we want to be presidents
we want to be governors
we want to be all of these things
ambition is good
just like people are ambitious who those in business
they want to be ambitious and to see how their business grows
but I pray and I appeal to you today
don’t let those ambitions of yours
overshadow our ability to fix those things that will help you to achieve your ambitions. ehm?
hii hapa hatuongei juu ya mtu.
kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye anaijua ile iko ndani ya roho ya kila mkenya
na yeye ndiyo tayari hata sasa tukiwa hapa yeye pekee ndiyo anajua rais wa tano wa jamhuri ya Kenya ni nani.
hakuna mwingine anajua
kwa nini sasa tumalizane hapa kwa sababu ya mambo ambaye hatuelewi
si turekebishe yale Mungu ametuwezesha turekebishe
hiyo ingine wakati wake ukifika
twaona tu kama ile ilikuwa juzi, huyu hee hu..
na tujue inafanyika wacha wananchi wakule mali wafurahie
wasikie maneno ya watu watachagua ama niaje wenzangu?
ama niaje?
si ni hapo?
kwa nini twaz…
sasa ni kutengeneza uwanja tunatengeneza
ni kutengeneza tunatengeneza kusafisha … eh?
ndiyo wachezaji wakuje baadaye
wawe wamepata kiwanja… ni safi, eh?
na wakenya sasa wanangojea mifuko ifunguke
na wakenya wanaheshimiana ikiwa ni Kibera wanaulizana
sasa wewe ujue wewe ukipanga upande hiyo ili utapata
ujue jioni tutakutana kwa mama Njeri
wewe ulete nusu mimi nikuambie ile tulipata leo
hiyo ndiyo siasa tunataka, ehh?
mama Acheng anajua ya kwamba stoki ya samaki sasa mwezi huu lazima niongeze eh?
kwa sababu kazi itakuwa safi eh?
na biashara ni nono lakini
haongozwi ni hofu ako na imani ya kwamba
katika wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
mama Atieno mama Chelagat mama Njeri wote wanajua
we are safe
we have nothing to fear
we shall wake up in the morning, vote, go back,
and continue our business and life will continue
I believe that is what each and everyone of you is desiring, au ni namna gani?
na ndipo niwasihi wenzangu someni hii kitabu
someni kila mmoja
lete maono yako
ambaye unafikiria inaweza kuchangia na kuongeza zaidi yale ambao hawa wazee wametuletea
najua Junet amesema ati anangojea baba asome
wewe Junet usiharibu watu bwana.
baba atasoma na atatoa maoni yake
hata Uhuru atasoma na atatoa yake
wacha watu pia wasome na watoe yao
yetu ni kupokea maoni ya hiyo watu yote na tuweke pamoja
na yule mtu ambaye pia ningeshukuru nimependa
pia vile ndugu yangu James ambaye ako na deni yangu
ee amesema ya kwamba wakenya ni rahisi sana siyo ngumu
ni rahisi sana kupata kitu ambacho tuko na tofauti kati yetu
hiyo siyo ngumu
ni ngumu zaidi kutafuta yale ambaye yataweza kutuunganisha
wenzetu Kenya hii hatutaitengeneza na siku moja
let us not to waste our time and our effort on those things that divide us
but let us create and put our energies to those things that put us together
so that those things that maybe we don’t agree on
we can put them to the people in an election
in a peacefull manner and the people can choose
between this idea and that idea
between this policy and that policy
that is why democracy strive
let us focus ourselves on that which puts us together
let us focus ourselves on those things that will make sure
we are more cohesive as a society
as the foreign minister of Tanzania has told us here
let us focus on those things that remove ethnicity and the sting of negative ethnicity
I am very proud of our culture, very proud of it
and I think we should be proud that as a country, we have 42 different, if not 46 now.
different cultures that we should be proud of that we can learn about
lakini, tusi-allow those wonderful, positive things about our culture
to be used and to be turned into instruments and weapons
of hatred and division
tunaelewana?
tunaelewana wenzangu?
hii tujivunie ukenya wetu, tujivunie utamaduni wetu, tujivunie lugha zetu
lakini, tusizitumie kwa njia ya kuweka chuki na mgawanyiko kati ya wananchi wetu
na ndipo mimi kama kuna kitu ingine hapo mimi nimeunga mkono
wajua tukienda Krismasi kwa muda huu wote
tunasherehekea siku yetu muhimu siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu
lakini sisi wote pia tunajua ya kwamba siku ile inafuata pia ni… ni holiday.
na tunaita boxing-day
na hakuna mtu mmoja hapa nataka mmoja ainue mkono aniambie boxing-day ni kumaanisha nini
boxing-day ni wakati wazungu wakati wanapatiana mazawadi zawadi wakati ya Krismasi
wanaenda kufungua ma-box kujua mtu amepatiwa nini kufungua …
sasa sisi hiyo siyo utamaduni yetu hiyo ni ya wazungu jameni
au ni namna gani?
so, mimi sioni ubaya jameni
tukisherehekea siku ya kuzaliwa Mwokozi wetu Yesu Kristu
na siku hiyo ingine tusherehekee utamaduni wetu kama wakenya
kwa sababu hiyo ni kitu that is Kenyan
so safari moja mtu ametoka upande ya Busia
anaweza kuambia jamii njooni hii siku tutembee Kisumu
tukaone utamaduni wa watu wa Kisumu
mtu ya Kisumu ametoka hapo
aseme mimi nataka kwenda mlimani kule Nyeri
nikaone utamaduni huko na hawa wanaishi namna gani
mtu wa Nyeri atoke hapo aende Mandera
aone hiyo watu upande wa Mandera
utamaduni wao uko namna gani
mtu mmasaai atoke hapo aende kule baharini
amezoea ng’ombe sasa aone samaki kubwa wanawala watu huko, eh?
tunaelewana?
let us celebrate now those beautiful and wonderful things
that are great about our culture.
and I promise you we will have a great country
we will have a firmer country
and as my brother Raila has said
this is not about Uhuru
this is not about Raila
this is not about Ruto
this is not about Kalonzo
this is not about Mudavadi
this is not about Wetang’ula
this is not about any of those leaders
this is about you and me
as Kenyan citizens
wenzangu, tuende, tusome, tujadiliane kati yetu mwezi huu
ambapo tunaelekea siku kuu
tutafute nafasi labda mwanzo wa mwaka u… mpya
tuje tukae tuone hiyo maoni
na ndio mimi nasema
let us own it mashinani
let us own it at the grassroot
si ni hivyo wenzangu
let us own it at the grassroot
let it not be niliambiwa na Uhuru
mimi na bibi yangu na watoto wangu
na jirani wangu tumeketi tumeongea tumeona
hii na hivyo ndivyo tungependa dunia yetu iishi
ni wangapi wanakubaliana na mimi jameni
tunakubaliana? tutatembea pamoja kama wakenya?
ndugu waheshimiwa, na waheshimiwa ma-MCA
jameni tumekubaliana ya kwamba
hii sijui Tangatanga, sijui Kieleweke
sijui warembo na huyu, na warembo na yule
tuachane sasa ni warembo wa Kenya
na viongozi wa Kenya
wakifanya kazi pamo…
(mwitiko: pamoja)
… ja, au ni namna gani?
si ni hivyo?
tumekubaliana jameni tutatembea hivyo
tu… tujadiliane halafu tuje tukutane hapo baadaye
tuone hiyo maono yooote na tukubaliane barabara ambaye tutatembea
mimi nasema Mungu abariki jameni
(makofi)
siku ya leo twasema
hongera kwa akina mama
kongole kwa wazee
na hiyo ingine ilikuwa gani? (akamgeukia mwingine)
na pongezi kwa wote
Mungu awabariki na walinde, asanteni sana! kwa heri ya kuonana!

 

ynshen