[FULLTEXT] Hotuba Ya Rais John Magufuli 2021/01/08 Baada Ya Utiliaji Saini Wa Ujenzi Wa Reli Ya SGR Mwanza-Isaka

HOTUBA YA RAIS JOHN MAGUFULI BAADA YA UTILIAJI SAINI WA UJENZI WA RELI YA SGR MWANZA – ISAKA

2021/01/08 Chato

Jamani, habari za asubuhi?
Mheshimiwa waziri Wang Yi,
Waziri wa mambo ya nje kutoka China,
mheshimiwa profesa Kabudi, waziri wa mambo ya nje kutoka Tanzania,
Waheshimiwa mawaziri wote mlioko kwa upande wa Tanzania
na mawaziri upande wa China
makatibu wakuu, watendaji mbalimbali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,
na wakuu wa taasisi mbalimbali mlioko hapa, nami…
[ukalimani]
Nami napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza
kampuni ya Kichina iliyoshinda tenda ya kujenga kilomita 341
za ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka
Na mimi nina matumaini kwamba watafanya kazi kwa uadilifu mkubwa
[ukalimani]
Mheshimiwa waziri wa mambo ya nje kutoka China alileta ujumbe
kutoka kwa rais Xi Jinping wa China kutuletea sisi Watanzania.
[ukalimani]
Na hii ni kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China
ya tangu mwaka wa 1964, 1965 wakati waasisi wa mataifa haya
Mwl. Nyerere pamoja na Mao Zedong walivyoweka maelewano mazuri
na kuwezesha uhusiano huu wa nchi mbili kuendelea kikamilifu hadi leo.
[ukalimani]
Ujumbe wa kutoka rais wa China, nimeupokea.
Lakini na mimi nimetuma ujumbe mwengine kule amfikishie mheshimiwa rais wa China.
[ukalimani]
Na mimi katika makubwa uliyomueleza ni kuhusu kuendelea kushirikiana katika nchi hizi mbili katika maswala ya kiuchumi.
[ukalimani]
Nimemuomba watusaidie katika miradi mitatu mikubwa ambapo ni ujenzi wa hydroelectric power kule Njombe, Lumakari, pamoja na Luhuji, majina ya Kihehe.
Lakini pia nimemuomba watujengee kilometa 148 kule Zanzibar za Highway.
Na hili amelisema wanakwenda kulishughulikia na atafikisha ujumbe kule.
[ukalimani]
Lakini pia nimemuomba wakatusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa.
Moja ya deni ambalo tunadaiwa ni milioni 15.7, za deni tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA.
Lakini kuna deni pia la nyumba za maaskari wetu ambao wamekuwa wapiganaji wazuri
na wameshiriki katika misheni mbalimbali za kimataifa ambalo
nyumba zile zinahusu karibu dola milioni 137 na tumeshalipa zaidi ya dola milioni 164
Lakini deni lingine ni la Urafiki, kiwanda cha Urafiki, dola milioni 15.
Haya nayo nimemuomba wakatufutie tu kwa sababu nchi ya China ni rafiki yetu lakini pia ni nchi tajiri.
[ukalimani]
Na mheshimiwa waziri amesema atalifikisha hili ombi China.
[ukalimani]
Ili waangalie namna ya kuweza kutusamehe na hasa katika ma-sheria zao za concessioning huwa ni kazi kubwa kusamehe madeni lakini wamesema watalifikisha kule.
[ukalimani]
Lakini nilimueleza urafiki wetu wa kati China na Tanzania ni mkubwa sana ndiyo maana leo tumeshuhudia utiaji wa saini hapa wa gharama ya dola za marekani bilioni [sahihi: trilioni] 1.32 ambao ni sawa na trilioni 3.026.
[ukalimani]
Na uhusiano huu umekuwa siku nyingi na ndiyo maana mheshimiwa waziri ameeleza hapa kwa miaka kumi iliyopita makampuni yaliyofanya kazi za ujenzi katika nchi hii yamechukua fedha trilioni 21, sawa na dola bilioni 10.
Na zimelipwa na walipakodi Watanzania. Huu ndio uhusiano na huu ndio undugu.
[ukalimani]
Kwa hiyo nina uhakika hata yale maombi yangu yatasikilizwa vizuri kwa sababu makandarasi wameshachukua trilioni 21 katika siku 10 tu, katika miaka kumi tu.
[ukalimani]
Lakini kubwa lingine ambalo tumezungumza tumeeleza uhali halisia kwamba China ni nchi tajiri humu duniani.
[ukalimani]
Na sisi Tanzania tuna mazao mengi ambayo tunaweza tukayapeleka China.
[ukalimani]
Na ndiyo maana katika zawadi zangu nimetoa korosho,
nimetoa majani ya chai, nimetoa kahawa nikiamini kuwa
sisi Tanzania tuko milioni 60, Wachina wako bilioni 1.4 hadi 5, wakila tu nusu kilo ya korosho zetu maana yake watakuwa wanakula tani milioni 750. Korosho zote za Tanzania zitakuwa zimeisha nafikiri hata za Afrika nzima.
Kwa hiyo iwe kitambulishwe kwamba wakaanze kula korosho za Tanzania badala ya kununua korosho sehemu nyingine.
[ukalimani]
Kwa hiyo nitoe wito kwa Watanzania wenzangu huu ndio wakati wa kulishika soko la China, kwa sababu, idadi ya Wachina iliyoko katika dunia ambao ni bilioni 1.5 inazidi idadi ya waafrika wote katika Afrika ambao tuko bilioni 1.2.
Sisi tuko milioni 60. Mazao yetu tuwe tunapeleka kule. Kama ni pamba, tupeleke kule, kama ni kahawa, wote wakanywa kijiko kimoja kimoja ukizidisha vijiko bilioni 1.5 utajua utakuwa umeuza kilo ngapi.
Tupeleke mihogo yetu, tupeleke samaki wetu, tupeleke mazao yetu
na hasa mazao ambayo tume-add value.
Nina uhakika kwa kutumia Wachina, uchumi wa Tanzania utapanda sana sana.
[ukalimani]
Na hii ndiyo faida ya kuwa na watu wengi.
Na mimi mimemuhakikishia kufanya biashara na Tanzania atakuwa amefanya biashara na Afrika Mashariki ambapo tuko watu milioni 165.
Lakini atakuwa direct amefanya biashara na SADAC ambako tuko zaidi ya watu milioni 400 hadi 500.
Kwa hiyo karibu zaidi ya watu milioni 500 atakuwa anafanya nao biashara kwa kufanya biashara na Tanzania, kwa sababu sisi ni wanachama wa nchi hizo.
[ukalimani]
Kwa ujumla, taarifa tuliyoletewa na mazungumzo tuliyoyafanya yalikuwa mazuri.
Na nimemuhakikishia kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu China ni ndugu zetu.
[ukalimani]
Baada ya kusema haya niwatakie mafanikio mema, niwashukuru sana waliofuatana na mgeni wetu ndugu Wang Yi pamoja na ubalozi na wengine wote waliokuja.
Lakini niwashukuru sana mawaziri na watendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wa kiongozi wana mheshimiwa Profesa Kabudi kwa mazungumzo mazuri waliyoyafanya.
Na nina uhakika wamefikia muafaka wa mambo yote.
Sasa ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote na kuonyesha ushirikiano mkubwa sana.
[ukalimani]
Mheshimiwa waziri, karibu sana. Ndugu walikwa wote karibuni sana. Xiexie.
Nafikiri chakula kitakuwa kiko tayari, twendeni tukale chakula ili kusudi tuendelee na mambo mengine.
Ninawashukuru sana pia kwa kuja hapa Chato.
Lakini nitoe wito kwa kontrakta ahakikishe hiki kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka kinafanywa kwa haraka zaidi, lakini pia niwaombe kama ombi lilivyotolewa na mheshimiwa waziri kwa serikali ya China.
Katika kipande hilichobaki cha Isaka hadi Makutupora.
kama wataweza hata kutukopesha kwa Concession,
sisi tutafurahi sana ili kipande kinacho kiweze kujengwa kwa sababu kitasaidia sana katika kujenga uchumi wa nchi yetu.
Na baadaye tutaendelea na Tabora hadi Kigoma na maeneo mengine.
[ukalimani]
China oyee
[ukalimani]
Xi Jinping oyee
[ukalimani]
Tanzania oyee
[ukalimani]
Wang Yi oyee
[ukalimani]
Ahsanteni sana ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.
Ninampongeza sana mheshimiwa Wang Yi anajua Tanzania hatuna Corona.
Ndiyo maana hakuvaa hata yale mabarakoa.
Ahsante sana mheshimiwa Wang Yi.
[ukalimani]
Ahsante sana nashukuru sana na mimi kwa kumthibitishia nakwenda kumshika mkono twende tukale chakula pamoja.

 

ynshen