CHENZA
1
Chenza kwetu kawaida,
Vichochoro lauzika,
Nikila kama ziada,
Fukuto nalo lashuka,
Ikiwa kinga ni mada,
Kiseyeye chazimika,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
2
Chenza tunda la magwanda,
Moja bei chini Kwacha,
Alilaye hulipenda,
Hatosheki kuliacha,
Lilwao watu na kenda –
Wanyama wenye makucha,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
3
Chenza pia lasafiri,
Wapi na wapi lendapi?
Ilivyo kubwa bahari,
Nani afunga halapi?
Hwenda Mamanga hodari,
Tena Wareno wafupi,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
4
Chenza pia ana ndugu,
Limau ‘sinilaumu,
Hizaya, chira na sugu,
Kula ‘furutu ni sumu,
Ila dawa ya mabugu,
Mvinyo mwa mlizamu,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
5
Chenza ‘kawa na mtoto,
Jina kupewa ni chungwa,
Chungwa ladhaye kitoto,
Aloshiki’ya Mwanangwa,
Ningampa maguruto,
Hofu sana longwalongwa,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
6
Chenza visa kuumana,
Mlimwengu nakwambia,
Kwamba langu kubwa mbona?
Jeuri ‘liulizia,
Jawabu kwa kweli sina,
Tabia nchi na mwia,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
7
Chenza ‘lojali ni nini,
Hata mie silijui,
Sinini wala sinini,
Bora pia hutambui,
Mdau awe chomboni,
Pasipo pepo hashui,
Chenza huliwa na nani,
Walimaji hawajali.
na Mroho Sinini
—–
CHENZA / 橙子~ 橙仔 [tʂəŋtsɑ]