2025年10月17日,内罗毕 Nyayo 国家体育场 (Nyayo National Stadium) 为 Raila Odinga 举行国葬时前总统 Uhuru Kenyatta 所作演全文:
视频链接:https://www.facebook.com/watch/?v=796698076503388
Asanteni sana
Asanteni sana
Mama. Mama Aida Odinga, Rosemary.
Asanti sana nimeshukuru, thank you.
Asanteni sana. Asanteni Asanteni
Nianze tena niseme Mama Aida Odinga, Rosemary, Junior, Winnie na familia yote ya mwendazetu rafiki wetu Mheshimiwa Raila Omolo Odinga
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoi Ruto na First Lady Mama Rachel Ruto, viongozi wa nchi za kigeni na majirani ambao wametutembelea kuja kuomboleza na sisi, waombolezaji wenzangu, hamjambo!
(Hatujambo)
Hamjambo tena!
Asanteni sana!
Tuko hapa pamoja kama wakenya, kusherehekea maisha ya mkenya mwenzetu kiongozi, rafiki yangu, lakini nilimpenda kama ndugu yangu.
Mheshimiwa Raila Omolo Odinga vile tumeambiwa hapa tulimjua kwa majina tofautitofauti. Agwambo, Jakom, Tinga, lakini kama wakenya, kutoka kona zote tulimjua tukamuheshimu kama baba.
Na tulimwita baba kwa sababu mheshimiwa Raila Omolo Odinga alipenda nchi yake Kenya kuliko kitu kingine chochote.
Mheshimiwa Raila Omolo Odinga, alikuwa baba wa wote, hakuwa na ukabila, na alipenda nchi na wananchi wa Kenya wote.
Na testimanti hiyo yaonyeshwa na marafiki tofauti tofauti ambao ukienda kumtembelea kwake nyumbani ulikuwa uliwakuta huko, marafiki kutoka kila kona ya taifa letu la Kenya.
Raila alikupenda kwa sababu ya maono yako, alikupenda kwa sababu ya fikira zako, alikupenda kwa sababu ya vitendo vyako, lakini siyo kwa sababu ya rangi yako ama kabila lako.
Leo hii, Kenya imepoteza kiongozi, kiongozi ambaye, historia ya demokrasia katika taifa letu la Kenya, haiwezi iandikwe bila la jina la Raila Omolo Odinga kuwa nambari moja.
Historia ya Kenya ya kutetea haki za kibinadamu na haki za wananchi wote haiwezi iandikwe bila jina la Raila Omolo Odinga kuwa nambari moja.
Historia ya ugatuzi na kuhakikisha kwamba wananchi kule mashinani wana uwezo ya kujiongoza na kujitawala na kuwa na viongozi ambao wanatekeleza shida za wananchi kule chini haiwezi iandikwe bila ya jina la Raila Omolo Odinga kuwa nambari moja.
In short nasema vipi, nasema hivi: Raila ametuacha kimwili, lakini ndani za roho yetu, ndani ya spirit ya Kenya, ataendelea kuishi miaka na miaka tukisonga mbele.
Wenzetu Raila alipenda amani, Raila alipenda umoja wa taifa letu, Raila alifurahia akiona wakenya wakiungana wakishirikiana wakijenga taifa lao pamoja.
Raila, alikuwa mtetezi wa haki ya kila mtu, pahali ambapo alikuwa anaona hakuna haki, Raila ndiyo alikuwa wa mbele hapo kuhakikisha ya kwamba haki zimepatikana.
Na wenzangu, wenzangu, nawaambia hivi: Tunawakumbuka wakina Mzee Jomo Kenyatta na Jaramogi Odinga kwa kutetea uhuru wa nchi yetu. Na kila mara, na kila mara, tukiimba wimbo wa taifa, tunasema tutalinda uhuru wetu na damu yetu na jasho yetu. Leo hii, tukiwa tunaaga baba yetu Raila Omolo Odinga nataka pia tujiape ya kwamba hatutakubali kama wakenya, haki za kibinadamu, demokrasia, na mambo yale yote ambaye Raila alitetea hatutakubali yarudi nyuma.
Hatutakubali yarudi nyuma. Tutasonga mbele tukizingatia hizo haki, kwa sisi ambao tumebaki na wale ambao hawajazaliwa. Hivyo ndivyo ndugu yetu angependa kuona na hiyo ndiyo njia ya kuona legacy yake kama kiongozi wa taifa letu.
Wenzetu sina mambo mengi, nimekuja kuomboleza rafiki na ndugu lakini siwezi nimalizie nisiposema ya kwamba hata kama leo tuna huzuni na tunaomboleza lazima kama wakenya tuchukue nafasi hii kwa sababu Raila hangeweza kutenda yale ambayo alitenda kama angekuwa amesimamiwa na mama nguvu wa kazi mama Aida Odinga na watoto wake Rosemary, Junior, Winnie na familia yake yote, kwa wakenya tunawashukuru kwa kutupatia Raila atumikie nchi na kwa kumuunga mkono ndiyo awe na nguvu ya kututumikia sisi wote.
Yangu ni kusema ndugu yangu uende vyema, hee, wenzangu, kastori kadogo tu siyo kubwa. Mnajua hee, unajua saa ingine baada ya kazi tukiwa tume- tulia tulia kidogo hapo tunapewa kakitu kidogo kidogo hapo… kwani… mnacheka mimi kakitu kidogo nasema uji na chai, eeeh.
Lakini wakati tulikuwa tunapiga gumzo, saa ingine tulikuwa tunajiuliza “unajua jameni wale wazee ambao wameenda wakina Jaramogi wakina Jomo wakina Nkurumah wakina Mwalimu Nyerere, jameni unafikirianga wakiketi wanaongeanga mambo gani?”
Mimi nilikuwa nasema “unajua wanaongea siasa kama sisi wanatuangalia tu mambo hii yetu ya upuuzi hapo, wanatuchekelea” Anasema “Eh, lakini unajua I’m very keen kujua” Sasa ndugu yangu umeenda mbele yangu. Sasa tiyari najua mmejua mmejiongeleshana huko. Na siyo ati niko na haraka ya kuja kuwafikia lakini heehee, bado tunataka tutulie tulie kidogo Mwennyezi Mungu atusaidie lakini najua wakati wetu tukifika utakuwa hapo kutuambia njia ya kutembea hizo ma-barabara za huko.
Kwa hivyo yangu ndugu yangu nikuombee Mwennyezi Mungu akurehemu akulaze na amani na wenzako. Ukijua ya kwamba twakukumbuka wewe na yale ambayo umebakisha tutaendelea nayo na familia yako sasa imekuwa yetu, na tutaendelea kuwalinda na kuwachunga na kusimama pamoja nao kwa wakati wote.
Nasema lala salama ndugu. Mungu awabariki familia yako na awapatie awafariji na wapatie nguvu na Mungu aendelee kuibariki Kenya hii yetu Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Asanteni sana Mungu awabariki.