[Makavazi] Mahojiano ya Hussein Issa Tuwa, rais wa UWARIDI, na ITV, Tanzania, mwaka mpya wa 2021

https://www.facebook.com/187353645175928/videos/410301496947059

下载:HusseinIssaTuwa&ITV

[KUNAKILI KUANZIA 00:53]

Moderater (baadae kwa kifupisho cha M): Hussein Tuwa karibu sana hapa ITV. Hapa inaonyesha kwamba wewe ni Rais wa UWARIDI. UWARIDI kwa maana ya nini? UWARIDI ni kitu gani?

Hussein (baadae kwa kifupisho cha H): Mimi ni urais wa UWARIDI ambao ni umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira Tanzania.

M: Umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira?

H: Unajua UWARIDI kuna waandishi wa riwaya halafu kuna waandishi wa riwaya wenye dira kuna tofauti yale. Sasa sisi kwenye UWARIDI tumejipambanua kwamba tunafanya uandishi wa riwaya lakini kwa malengo mahsusi ya kuisogeza kwanza fasihi ya Tanzania mbele, kuiweka juu ionekane lakini vile vile nasisi waandishi wenyewe tuweze kunufaika kwa kazi za mikono yetu kwahiyo tunavofanya vitu tunakwenda kwa malengo tunakuwa tuna dira maalum ya kutuongoza. siyo tunaandika, kwa waandishi miongoni mwa waandishi tu hapana ni waandishi wenye dira tunaandika kwa malengo, tunaandika kwa ueledi, tunaandika kwa kufuata maadili, tunaandika kwa kuwa na utaratibu mahsusi ambao tunaamini tukifuata ule utaratibu tutafika kule tutakapofika, au tutafikisha fasihi ya Tanzania kule inapopaswa iwe.

M: Bado nashawishika kujua zaidi katika hii dira, labda unipe mifano katika dira ambao mnakusudia labda uandishi wa zamani ulikuwa hivi, ama waandishi wengi wanafanya hivi, hiyo tofauti UWARIDI katika dira ambayo unazungumzia tumetoka hapa tumekwenda hapa.

H: Swali zuri sana. Unajua UWARIDI imekuja katika kipindi ambacho waandishi wa riwaya wanaonekana kama vile ni vitu duni, kitu ambacho hakijatiliwa maanani, kitu ambacho labda tuseme cha watu wa kale ambacho kimebakia, ukiwatazama waandishi wale wa zamani, kina Musiba, Ben Mtobwa marehemu?

M: Vitabu makapi?

H: Yes. Ndiyo UWARIDI imeingia pale. Sasa sisi tukasema tunakuja tubadilishe hii. Inabidi tuonekane kwamba kwanza vijana wanaweza kuandika vile vile lakini vile unavyoandika mambo ambayo ni ya kisasa ya kwenda wakati uliopo, ile peke yake ni dira. Kwa hiyo ndiyo pale UWARIDI ulipoanzia. Kwa hiyo hii ndiyo dira yetu ikawa “tutafanya nini?” Kwanza, tuifanye fasihi ya tanzania ya uwandishi uonekane upo na ufahamike na uheshimike. Kwa hiyo tukaja na dira ya kufanya matukio matamasha ya vitabu uzinduzwa vitabu mijadala ya vitabu, kuweka pamoja waandishi na kupeana elimu ya ubora wa kuandika, namna gani waandike kazi siyo bora kwahiyo ilikuwa ni dira, kidogo kidogo tumetajiriwa mpaka ikawa sasa imetufikia hatua sasa ili kusema: ahh, waandishi wa riwaya bongo bwana? Hii inaweza ikawa na nguvu kwa sababu tunaweka weledi pale UWARIDI. Tumeweka, tumefuata misingi ya uandishi. Siyo vile mtu kwa sababu unajua kuandika unatuma kazi kwenye mtandao unatoa kitabu na unapeleka kwa wasomaji lakini tulikuwa tunafuata maadili. Unapeleka kwa mhariri, unahakiki, unafanya vizuri, unatengeneza jalada safi, unaona? Unatoa nakala za kutosha

M: Kusiwe na ukakasi?

H: Siyo kwamba ukakasi kwa sababu inapaswa zile kazi ziheshimika sasa. Lakini siyo hivyo tu. Kwa kufanya view sasa tumeweza kupeleka, kunyanyua. Mpaka sasa. Fasihi yetu kwamba sisi tumefanya pamoja na Kama hawajui tuko watu wachache sasa Kuna wengine ambao walikuwa wanalegalega, wakaingia nao hawakufanya. Ilikuwa ile ile kwamba “aya kumbe kama hao wanaweza kwanini tusifanye”. Kwamba matokeo yake jamii pana sasa ya fasihi ya Tanzania inanufaika.Wasomaji wana… wanaona kumbe “sasa vitabu tunapata”, wanaweza kusoma. Imefikia hatua sasa hivi. Mtanzania haoni haya ya kutembea na kitabu cha mwandishi wa riwaya ya kiswahili mkononi.

M: Hata kwenye daladala anaweza kupanda nacho hana wasiwasi kwamba anaweza kaumbiwa “achiaaa.”

H: Hana wasiwasi. Halafu basi, kipindi kile huko ukitaka uonekana umesoma upite na vitabu vya wazungu kama vya James Hadeley Chase, ndiyo maarufu kwenye daladala.  Ukionekana kushika hicho huyu jamaa ni msomi sana.

M: Ili ionekane kwamba jamaa yuko vizuri.

H: Ee, Ndiyo ilikuwa hivyo umeona lakini sasa hivi. Vitabu vyote vina kama hivi mkimbizi, unaona fumbo. Watu wanasoma[ unaona? ] Vitabu vya waandishi wa kitanzania. Mtu anashika hana wasiwasi na hiyo sasa. Ndiyo dira sasa. Imefika sehemu sasa imeibua hata wale wasomaji wambao walikuwa huko wamejificha hawajui watapata wapi vitabu wamerudi sasa. Wamekuja na wameona jinsi vitabu vinavyopatikana hiyo sasa ndiyo dira.

M: Nakumbuka tulizungumzia wasomaji wa vitabu 2021. Huwezi ukazungumzia mwaka wa 2021 bila ya kuzungumzia mwaka wa 2020.

H: Kabisa.

M: Kwa sababu ukijua kuwa umetoka wapi ndiyo utajua kwamba kukoka huku nilipotoka nakwenda huko. Kama nilijikwaa sehemu Fulani au kitu gani kilinifanya nianguke ili mwengine akija asijikwae.

H: Sawasawa

M: Kuna lile swala uchapishaji.

H: Ndiyo.

M: Mara nyingi, imekuwa ni changamoto kwa waandishi wanaoingia. Kwamba kuna mtu ameambiwa wana warsha wa kuandika vitabu. Unaandika kitabu chako halafu na ukapeleka kwa mtu kuchapa na unachapa. Baadaye ndo kama kuna chochote kile, ndo wakuletee kama mia ama mia mbili. Kwenye hili ukisalia mpaka pale katika dira. Lakini kwenu nyie mnajitazama namna gani? Na dira ambayo mko nayo?

H: Toka mwanzo, tulivyoanzisha UWARIDI, dira yetu sisi ni kuwa tunaondoka kwa katika masuala ya utendaji wa namna hiyo kwenye vitabu. Kwa sababu tumeshaona kwamba hii ya kumkabidhi mchapishaji. Achukue nimpe kazi yangu, yeye ndiye editor, a[u?]fanye layout, utafute soko, auze halafu mwisho wa mwaka, anilipe ile asilimia kumi, tumeona haitufai Siyo nia/dira yetu hiyo kwa sababu saa hizi tunataka tupate kazi iliyokuwa bora na tunufaike na kazi tuliyofanya, hii ndiyo kama dira tunayofanya katika uandishi. Kwa hiyo, tukasema tuwe na kitu kitakachotuongoza kama dira. Kwa hiyo tukasema sisi kama UWARIDI dira yetu itakuwa ni kuwekeza kama waandishi.

M: Tuambie kidogo juu ya TUZO? Kuna mwandishi Maundu eeh.

H: Kuna Maundu eeeh, huyu bwana naweza nimpongeze, hiyo ni kazi nyinginezo ya timu ya UWARIDI. Anafanya kazi nzuri sana.

M: Yuko vizuri.

H: Na anachokifanya ndiyo kazi ambayo anatakiwa kufuata katiba ya UWARIDI. Lazima yeye atoke aongee na watu mbalimbali au na vyombo vya habari?? kwenye mtandao. Anaifanya vizuri. Na tulikuwa na wengine tuwafanye waishike nafasi lakini hawakuwepo na level hizo

M: Kongole bwana Maundu Mwingizi

H: Nampongeza sana. Kijana wangu nampongeza

M: Kama rais anakupongeza, ndugu yangu, basi

H: Anafanya kazi nzuri sana. Kazi si nimemtuma ataifanya. Kama kumtuma Si nimemtuma. Nenda kule, kausemea umoja (UWARIDI).

M: Ehh,

H: Kwa hiyo haturudi kwenye ile hali ambayo nimeizungumza.

M: Ehh

H: Kwa hiyo sisi tukasema sisi UWARIDI hatutokwenda kule. Sisi tutawekeza nguvu zetu, kwenye kutoa vitabu vyetu wenyewe, ili tuweze kupata vipato vyetu wenyewe kwa muda unaostahiki, siyo kusubiri mpaka mwaka ufike, unaona? Kwa hiyo tukaja na kitu cha kwanza tukaanzisha [hiyo ile] tunasema UWARIDI riwaya fund, mfuko wa riwaya wa UWARIDI. Ilikuwa ni kama jozi fulani hivi. Lakini tumejua ndio dira sasa vision. Tunasema hiki kitabu tutakitoa, tukafika? Tukaweka vipato vyetu pale. Tukasema jamani; sisi si ndiyo wanaUWARIDI? Hebu tuchange kila mtu laki mbili hapa, tutapata shilingi ngapi? Tumechanga huko tumepata milioni moja na nusu. Hii haitoshi kwa kumchapia ehm ehem Kamanda Amata kitabu? Hiyo milioni siyo tu kumchapia, itamlipa editor bora. Itamlipa mtu wa kufanya layout designer bora, Itamlipa mtu wa kutengeneza kava bora, italipa uchapishaji bora na italipa gharama za kukitangaza kwa kitabu kwa sababu lengo ni hela irudi.

M: Eeh!

H: Siyo tu ukitoa kitabu kikae kule usubiri. tunakitangaza, kwa nguvu. Tumeingia kwenye mtandao, tunaweka zile posts za facebook, hizi na instagram zinasaidia, huwa 15 au 30 ili watu wengi waone. Umeona? Tuna mbinu mbalimbali za kutangaza kitabu ili hela irudi. Hiv haiwezekani kweli? Hii inawezekana. Let’s do it.

M: Mm.

H: Dira sasa niliyokuambia, tukafanya vile. Tukamtea Kamanda Akata, tukafanya vile tukamtoa Laura Petite, Kiroba cheusi. Ni vitabu ambavyo amefanya kazi vizuri

M: Mm.

H: Dira ile Hakuna aliyewahi kufanya kitu hicho kabla. Kwa hiyo, umoja, nadhani unaona hicho Tumemtoa Lilian Mbaga na Hati Nafsi. Na sehemu tunafanya kazi nyingine. Kwa hiyo hii ndiyo dira. Kwa hiyo, tumeshatoka huko sasa.

M: Haya, na mtazamaji kama umeungana nasi ni raisi wa UWARIDI. Hussein Tuwa, ni mwandishi wa vitabu tunazungumzia usomaji wa vitabu wa mwaka 2021. Tunatazama tulipotoka tuambie tunakwenda wapi kupitia 0759 42 78 88 kama inavyoonekana kwenye runinga yako unaweza ukapiga simu sasa au kauliza maswali kwa siku hii ya leo. Amabao wapo kukutazama sasa, dira hii ya 2021 mnajipanga namna gani? Wakati tutafunga mwaka tukio kubwa ambalo lilifanyika ni uzinduzi wa kitabu cha TUZO

H: Ndiyo.

M: Ni UWARIDI ama ni nani [halafu] alifanya kazi ya kubuni kwa sababu tumeona nanyi mlikuwepo pale. Na kwenye jalada pia mnaonekana waandishi wengi ambao mko pale?

H: Swali zuri sana. Nashkuru kwa lilo swali. Uzinduzi wa TUZO siyo UWARIDI

M: Ehem.

H: Wazi kabisa, siyo UWARIDI. Uzinduzi wa TUZO, ni juhudi za waandishi wa TUZO ambao ni waandishi watano nikiwemo mmoja wao.

M: Ehem.

H: Sasa yale waandishi waliofanya huo uzinduzi wanatoka kwenye umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira. Lakini, ule uzinduzi – kama nilivyosema hii ndiyo dira yetu – kuanzia gharama za kuchapa kile kitabu, gharama za kukodi ule ukumbi. Nilienda nikaulizia ule ukumbi maana tulichofuata ni kuwa bei yake haiendi juu sana.

M: Ehmmmm.

H: Zile gharama za ule ukumbi, gharama za kutengenza jalada, gharama za kutengeneza zile poster za matangazo. Gharama za kulipia matangazo na zingine zote ni za wale waandishi binafsi fedha zao kutoka mfukoni.

M: Ehmm

H: zote!

M: Ehmm

H: Ni wale waandishi binafsi fedha zao za mfukoni, zilikuwa tunapigwa paso kwa paso divide by 5. Unagawanywa kwa tano. Kwa hiyo tuka.. kitambo tukiambiana milioni ngapi inagawanywa kwa tano. Kila mtu anatoa. Umeona? Tukikodi ukumbi ni laki sita? Inagawanywa na tano. Kila mtu anatoa. Sasa. Hiyo ndiyo dira sasa. Uwekezaji kwenye vitabu.

M: Kwa hiyo ijapokuwa ama miongoni mwa ambao wameandika, baadhi ni watu ambao kutoka UWARIDI

H: Ndiyo.

M: Lakini si jambo la UWARIDI

H: TUZO haiko UWARIDI kabisa. Hakuna shilingi ya UWARIDI iliyotumika pale. Lakini tunasema hivi. Sera yetu nyingine kwenye UWARIDI ni kwamba unapokuja kwenye umoja , usijiulize eti huu umoja unanifanyia nini?

M: Mmm

H: Njoo pale ujiulize mimi ndiyo nimefanyia nini umoja?

M: Ni kuona mbele zaidi.

H: Ehhe, umeona? sisi watano sasa tupo wapi? Tupo UWARIDI, Na sisi tunafurahi kwa hilo kwa sababu ndiyo lengo letu. Tukae kwenye umoja, upeane mbinu za kwenda mbele.sisi watano. Tumeweza kufanya hichi kitu. Na akili ilianza kama kitu tofauti kabisa. Kilianza kama challenge kwenye mtandao. Baadae watu wakaomba tuchape kitabu. aliyozungumza. Kwa hiyo. hata ilivyokuja kuchapisha kitabu.Baada ya watu kuomba ilibidi tutafutane sasa. Jameni hawa watu wameomba kitabu lakini je, tuko tayari? Inamaanisha kukubali maanake gharama!

M: Ehmm

H: Na sasa ukiona mtu ambaye dira imemshika, hasiti. Mimi naomba niwapongeze hawa waandishi wenzangu tulioshirikiana kwenye TUZO.Walikuwa na msimamo..

M: Ukiwataja siyo dhambi..

Yes. Nilikuwa na Fadhy Mtanga, Maundu Mwingizi, Lilian Mbaga na Laura Pettie

M: Hussein Tuwa.

Na kaka mkubwa Hussein Tuwa.Umeona kwa hiyo, mimi nilikuwa sina wasiwasi na uwezo wao wa kuandika na umuhimu wao wa dira. kwahiyo. [Ilikuwa ilivotaja] hakuna gharama hata moja ambayo mtu karudi nyuma. Kwa hiyo vile nilivyotaja, hakuna aliyesema, aaah, siwezi subiri. nimsubiri kwanza. Ilikuwa tukisema jamani nyie. Inabidi tupate hapa milioni mbili na laki nne. within 24 hours watu wameshaleta hela.

M: Huu mzigo tayari unaweza ukasaidia kufanyia kazi

H: Anajua yeye. Sasa huo. Unaona hiyo ndiyo dira tunayoisema.

M: Kwa sababu kama bila dira hakuna uthubutu ndani yake.

H: ndani yake? kuwa na waandishi wengine waige mfano wawe na . Ule moyo ?? swali lako la kwanza. Ule moyo kwamba. Nyie ndiyo kwa publisher nimpelekee kazi, nichapie bwana halafu ninamuomba. wewe mtumivu Eeh, kwa maana bila dira hakuna uthubutu ndani yake. Kuna waandishi wengine waige huu mfano wawe na moyo huo huo. Siyo kwamba niende kwa publisher nimpelekee kazi, anichapie, halafu namwambia …

M: Mwisho wa siku…

H: Eehmm

M: Unamwambia nitengenezee hii iwe hivi

H: Hivi…, hivi…, yes! Huko hatutaki sisi umeona? Yaani hunamkuta mwana-UWARIDI kwenda huko.

M: Naam.Tutazame sasa katika usomaji wa huo mwaka wa 2021. Tumeona mengi mwaka 2020

H: Hemm.

M: Sasa tupo mwaka wa 2021. Tumeona mengi mwaka 2020. Sasa kwa mwaka 2021 mnaweza kuona kuna kitabu kimepelea kwa wasomaji tukiongeze au kimezidi tukipunguze ili sasa wasomaji wavione vizuri?

H: Okay. Ahsante sana, kwenye 2021 kwenye usomaji, kwanza, cha kwanza kabisa, kwa sababu huwezi kusoma bila vitabu kuotoka.

M: hemm

H: Kazi tulifanya huku 2020 imetuongezea idadi kubwa sana ya wasomaji. Kwa hiyo 2021 tunabadilisha sasa idadi ya nakala za vitabu za kutoka. Kila vitabu idadi ya nakala itakuwa kubwa kuliko ile ya mwaka uliopita. lakini, hilo ni la moja, lakini la pili, idadi ya vitabu vyenyewe vitakuwa tutatoa vitabu vingi zaidi. ndiyo lengo kwamba 2021. Tumesema angalau kila mwandishi atoe katika mwaka huu mmoja vitabu vitatu. Tunataka tufanye hivi. Ina maana tukitoa vizuri tunauona UWARIDI wote.

M: UWARIDI wote

H: Mpaka sasa sehemu tumefika wanachama ishirini na saba ishirini na saba mwaka wa tatu. Na tumeshasema. Na tumeshasema kabisa sera tumeambiana ndani ya UMOJA kwamba ukipita mwaka hujatoa kitabu, inakubidi uitwe kwenye kamati tukuulize wewe Bwana, upo na sisi ama upo kwa kutuchungulia kufanya nini.

Tunataka tupeleke vitabu mbele. Tulivyoanzisha umoja Tuitoe katangazwe unakumbuka. Tuiweka tangazo kubwa kwenye facebook. Tusema tuna ndoto. Na lile tangazo lile kwenye facebook, picha yake. Ilikuwa ina vitabu vingi ambvyo vimefunguliwa hivi tukasema tuna ndoto. Na ndoto yetu ilikuwa ni kujaza vitabu nchini. Lile tangazo, baadhi ya watu walilielewa na baadhi hawakuielewa. Unajua Maundu, anasema kuna hii tabia ya nzi, nzi ana tabia moja ya kwamba kisafi hakifuati, halafu hapo kwenye kichafu kuna asali imemwagikia, basi watakuja hapo watajaa hapo watafanya mzozo brbrbr hapo na pia huyu jamaa ni mchafu kama nzi kweli. Uhmm umeona?

M: Siyo hii, kuna ile nyigine nitakuja

H:

M:

H: Kwahiyo, kwahiyo, eeem. Lengo la lile tangazo ni kuweka, from day one, kwamba dira yetu ni hii. Sasa ikaja sasa tunaweza kupata wapi hivi vitabu. Vitabu hivi lakini sasa tumefanya. Vitabu vinakuja na. Ile dira kwamba sisi tukifanya basi na wengine watafanya ijapokuwa siyo la UWARIDI

M: Lakini

H: Watafanya.

M: Wataunda umoja wao

H: Yes!

M: Na watatangaza kwamba vitabu vipo.

H: Eeh kama sisi kwamba sasa iwe neno kusema sijui kwamba Tanzania sijui hakuna wasoma vitabu. Hii kusema hakuna wasoma vitabu tunataka tufute ile. Lakini vile vile tunataka kitu kinachotuuma zaidi hapo. Kuwekeza

M: Dira.

H: Inakuja. Inafunguka Yes Kwamba tuumie ili kwenda na dira. Kwa hiyo dira yetu ni hivyo kwani vitabu na vitabu ya andiko la Tanzania la Kiswahili. Umeona? Kwa hiyo. Lengo ni kufikisha pale. Nafikiri tunakwenda kule. Tulikuwa tunasoma mtandao wa wikipedia, katika kuitafsiri Tanzania, kitu kigumu ambacho kilituuma sisi katika zile sifa za Tanzani kwamba sijui kwa Afrika Mashariki watu wake wana makabila kadhaa. Lakini, sifa moja yao ni kwamba watu wake sio wa kupenda vitabu na usomaji wa vitabu uko chini sana, na vitabu vikipatikana vinakuwa ghali sana

M: Hawajatutendea haki.

H: Hawajatutendea haki! Kuna mikakati gani. Na hii tutaona kwamba mtu hakuna haja ya Tanzania akisoma ile. Ina maana nanunua vitabu vyake havitatoka. Kwa sabau wenzetu wana tabia ya kusoma. Siyo? Anakuja anavyobeba mzigo mkubwa wa vitabu. Hiyo ilitukera sana. Ndiyo tukaja na Mjue Mtunzi. Ndiyo tulikuwa strategic yaani ni dira. Kwamba tunataka tuionyeshe dunia kwamba “Si kweli!”Tanzania vitabu vinasomwa na waandishi wapo.

M: Tukitazama kuwa katika hizo tasnia utakuta kuna fulani mlezi wa tasnia fulani. Au fulani ni mlezi wa kada fulani? Kwenye uandishi wa vitabu hili sijawahi kusikia. Hili likoje kama mwaka wa 2020 mlikotoka, na huu 2021 lile swala la ulezi likoje?

H: Swali zuri. Toka tulivyoanza UWARIDI tulijua kabisa ili tufike mbele na sera zetu hizi. Labda tukapa mlezi wa kitaifa ambaye atakuja kutushika mkono kutu…? Kwa hiyo toka tuanza UWARIDI tumeyapeleka maombi mengi sana. Wizarani. Kwa watu ambao tunadhani wanaweza kutusaidia. Lakini, kwanza hatuna aliyetujibu. Na iliyetujibu akaja kusema “nipeeni muda”. Halafu mpaka sasa, tunasubiri. Wote tukawa tunashangaa lakini, sisi, tunachotaka kukifanya watu wengi hawakielewi. Hawatuelewi kabisa.

M: Na ndiyo maana kwa sababu nipeni muda huu ayatazame hawa

H: Watutazame! Kwa hiyo tukasema sisi, lengo letu ni kuwa tutajiweka mbele tuonekane watu waone waone uwezo wetu, waone uwepo wetu. Watatujua na kitu tutakachoweza kufanya. Baadaye watatusikiliza. Tukasema tutafanya matukio makubwa ya vitabu nchini kuonyesha kwamba waandishi wapo na wanaweza, umeona, nao peke yake unajua kila unapoingiza dira kitu kipya mara nyingi kinakuja. Iwezawezekana vipi ile? Ukisikiliza hiyo kufanya kitu, ndiyo kitu baadaye nitataka kuvizungumzia ndiyo kwa waandishi wengine nao niwape isome, umeona? Si tukasema tutafanya, na tukafanya na tukaja “mjue mtunzi”tukio kubwa kabisa la kitabu kupata kutokea we shahidi, hakuna aliyewahi kuona tukio kama lile Tanzania la vitabu, limekwenda viral, worldwide, dunia nzima, letu lile. Na matokeo yake sasa, tukapata sisi taarifa kutoka Uingereza, kwamba “Bwana Tuwa, tunataka tuwaandike kuhusu tukio lenu, unasemaje?”

M: Eeh

H: Tukasema haina tatizo, ndiyo tuliwaambia waandika wanavyotaka! Sawa? Kilichofuata sasa Air Tanzania, kwenye gazeti lao, in-flight magazine, twiga in-flight magazin. Wakasema si tunataka tuliweke hili tukio lenu kwenye gazeti letu ndani ya ndege

M: Fomular.

H: Fomular. Unaona sasa? Dira. Tuko pale sasa. Sasa baada mambo yetu haya mwaka huu baada ya kufanya tukio la TUZO sasa. tunafunga mwaka ishirini. Nakuja kwa swala lako la ulezi. Mkuu wa mkoa Daressalam. Aboubakar Kunenge. Amekubali kuwa mlezi wa UWARIDI

M: Hongereni sana.

H: Umeona? Kwa sababu gani? Mkuu wa mkoa, ana vision kali. Ana dira. Si mtu wa kukubali vitu tu ovyoovyo. Utendaji wake unadhani unauona yuko tofauti sana, yuko makini sana. Amekubali fanya kazi na UWARIDI kwa neno pale kuwa mlezi. Anaona mbali. Ameona/Anajua, kwa sababu ametuona kwenye magazeti ya Tanzania.

M: Tunawatoa watu kwenye wakati ule unakwenda mahali utaambiwa waandishi wengine vigezo havikidhi, unaoana ni kama ishirini tu.

H: Sasa ninachotaka kukuambia ni kwamba. Unajua kitu kikubwa ambacho kimeifanya fasihi yetu ya uandishi iwe vile ilivyokuwa kabla UWARIDI haijaja ni uoga. Uoga wa kufeli. Uoga wa kuanguka. kwa dah, nikifanya hiki halafu nikishindwa itakuwaje. Sisi UWARIDI hatuna uwoga huo. Sisi tunadiriki kufeli. tutafanya tukio hili ituanguke, hatuogopi kuanguka. Kwahiyo tunasema tunapofanya tukio fulani sehemu fulani hatuogopi kuanguka, tunafanya wakija watu wawili.

M: Tumefanya.

H: Tumefanya.

M: Na ujumbe umefika.

H: Na ujumbe umefika. Sasa tumefanya matukio kama haya tunaona watu kama aah. tutaona kama tutapata watu, twende tukashuhudie. Sasa wale, ndizo waogope! Sasa mimi nawapa ujumbe sasa hivi waandishi wengine ambao sio UWADIRI. Nao waandishi wa WARIDI ambao bado wana mashaka mashaka, usiogope kuanguka. Tunasema hivi, Anguka, mara ya kwanza, Anguka vizuri mara ya pili, sawa ee? Anguka vizuri mara ya tatu. Mara nne usianguke.

M: Wakati mara ya nne asianguke hebu uwape namba ya simu. Namna ya kuwapata watu wa UWARIDI. UWARIDI mnapatikana vipi kwa namba ya simu. Mtu kama akitaka ushauri na chocohte kile, tuwape namba ya simu.

H: Kwanza unaweza kutupata kwenye mtandao moja kwa moja. Mimi namba yangu ninapokea simu 0764 49 20 55

M: Rudia tena.

H: 0764 49 20 55

M: Na kwenye mtandao wa kijamii, UWARIDI mnapatikana vipi?

H: Tunapatikana

M: Namba ya raisi inaonekana hapa nidyo hiyo.

H: Tunapatikana sisi kwenye facebook ukiandika tu “UWARIDI official ” utatuona tuko pale tumejaa tele. Utapata maelezo yote yetu utayapata. Ingia kwenye Instagram, “UWARIDI Official”, utapata maelezo yetu, ingia Twitter UWARIDI official

M: Ahsante

H: Tuko pale

M: Usiisahau ITV Super Brand Afrika Mashariki. Ahsante sana mimi naona kuna mengi hatujayagusa Nitakuita tena kuja hapa, tuzungumze kwa undani zaidi

H: Nitashukuru sana.

 

ynshen