[Makavazi] Hotuba na Samia Suluhu Nairobi, ziarani Kenya

2021/05/04 Nairobi

下载:墙外

|Nakushukuru Mh. Rais.
| Mh. Rais Uhuru Kenyatta wa  Jamhuri ya Kenya
| waheshimiwa viongozi wa Tanzania na Kenya mliopo hapa
| ndugu wanahabari, mabibi na mabwana
| nianze kwanza kumshukuru kaka yangu Rais Kenyatta
| kwa kunialika kuja kutembelea nchini kwake| Nakushukuru pia kwa makaribisho mazuri
| niliyopata mimi pamoja na liliyofuatana nayo
| toka tumetoka airport, mpaka tunaingia Ikulu
| tumepokewa vizuri sana njiani
| Mheshimiwa na ndugu wanahabari niseme kwamba
| muda mfupi uliopita tumetoka kufanya mazungumzo na Mh. Rais Uhuri Kenyatta
| tumejadili mambo mengi kama alivyosema mwenyewe
| ninalotaka kuliweka msisitizo
| ni lile linalohusu kukuza na kuimarisha
| uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili
| na hili ndilo jambo la msingi kama alivyosema
| Tanzania na Kenya siyo tu majirani lakini ujirani wenyewe ni wa kindugu
| alisema pia kwam ukiangalia mikapa inayozunguka Kenya
| mpaka wao watanzania ndio mkubwa kuliko mipaka ya nchi nyingine zote
| lakini kwenye mpaka huu
| wale wanaoishi mipakani wako Tanzania wako Kenya nao wote ni ndugu
| kwahiyo uhusiano wetu ni wa kindugu
| kama mnavofahamu nchi zetu mbili siyo tu majirani kama nilivyosema ni marafiki na ndugu
| na kutokana na urafiki tulio nao
| tumewezesha kukuza ushirikiano wa kiuchumi
| k.f. wakati wa mazungumzo yetu nimemuarifu kaka yangu Rais Kenyatta kuwa
| Kenya inashika nafasi ya tano kuwa uwekezaji wa ndani ya nchi ya Tanzania
| ikitanguliwa na mataifa mengi kutoka nje
| lakini ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
| Kenya ni ya kwanza na ulimwenguni inashika nafasi ya tano
| amapo imewekeza miradi 513 ya thamani ya USD 1.7 bilioni
| ambayo imetoa ajira zipatazo 51 000 za watanzania
| aidha, zipo kampuni 30 za Tanzania ambazo zimewekeza
| mtaji ndani ya Kenya wenye thamani ya Ksh 19.33 bilioni
| na kutoa ajira wa watu 2600 na kama 50 hivi
| lakini nikaweka ahadi kwamba
| Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote Kenya
| kuja kuwekeza, ili kukuza… kukuza ule ujazo wa biashara au /volume of trade/
| lakini mbali na uwekezaji nchi zetu mbili
| pia ni wadau wakubwa wa biashara ambapo kwenye miaka mitano iliyopita
| wastani wa biashara ni Tsh 1 trilioni au USD 450 milioni
| ambayo siyo kubwa na tumeweka ahadi kuikuza
| hivi basi mazungumzo yetu tumekubaliana
| uhusu namna ya kukuza biashara na uwekezaji kati yetu
| kama mnavyofahamu nchi zetu bado zina fursa nyingi sana
| ikiwemo kwenye maswala ya kilimo, viwanda, uvuvi, ufugaji na utalii
| tuna fursa kubwa sana, Mungu ametupendelea
| sasa tunakwenda kuzitumia fursa hizi kukuza biashara kati yetu
| lakini kati yetu na mataifa ya nje
| lakini kwa lengo la kukuza biashara pia
| na uwekezaji kati yetu, tumekubaliana
| kuendelea kushughulikia baadhi ya changamoto
| hususan vikwazo visivyo vya kodi
| ambavo vinatokea katika mipaka yetu
| tumekubaliana kwamba hivyo sasa vikaondoke
| na kwa pamoja tumeitaka tume yetu ya ushirikiano baina ya Kenya na Tanzania
| iwe inakaa na kutoa suluhu ya vikwazo vinavyojitokeza sasa hivi na halafu
| ili vikwazo hivi visiwepo
| lakini jingine aliloliingiza Mh. Rais na mimi nakubaliana nalo
| ni kuwa mawaziri wetu wa afya kukaa
| na kuangalia kurahisisha mfumo wa kuingia na kuchekiwa
| kwenye mambo haya yaliyoingia ya Covid au Corona
| watu wetu wapate huduma za haraka
| kupima, kuchekiwa ili waweze kupita na biashara ziendelee
| ndugu zangu wanahabari
| mbali na ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kwenye mazungumzo yetu
| na Mh. Rais Kenyatta tumejadiliana pia kuhusu namna kutekeleza miradi yetu ya kimkakati
| miradi inayohisi usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa
| lakini pia, jinsi ya kupata nishati,
| umeme au gesi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine
| una hiyo miradi, mmoja tulishasaini mkataba leo
| tunachokwenda kufanya ni kusimamia utekelezaji
| lakini pia kuna mmoja ambao unaendelea
| mazungumzo yako karibu kumalizika tuta…
| nitumie lugha ya Mh. Rais tuta/weka kidole/ hivi karibuni
| lakini pia na mwengine tuko kwenye mazungumzo kuumaliza
| tumegusia pia swala la ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Daressalaam hadi Mombasa
| huu ni mradi wa muda mrefu
| tunashukuru leo tume/weka kidole/
| na kilichobaki ni utekelezaji tutakwenda kuusimamia
| maswala mengine ni maswala ya kawaida ambayo tumezungumza
| na tumejadiliana kuhusu maswala ya ushirikiano kimataifa
| hususan namna kujiimarisha au kuimarisha Jumuiya yetu Afrika Mashariki
| ikiwemo kuzihimiza nchi wanachama kulipa michango yake
| hili nalo ni jambo ambalo linatusumbua kidogo ndani ya Jumuiya
| kwahiyo nalo tumesema tuhimizane tulipe michango ili Jumuiya iweze kusimama vizuri
| lakini pia kuna maswala mengine ya mipakani ameyazungumza
| na maswala mengine madogo madogo ambayo tumezee
| tusingekwenda1 kukaa na kuyafanyia kazi
| mwisho ni kwa taarifa yenu waandishi wa habari kwamba
| mwaka huu ifikapo mwezi wa 12 Disemba
| Tanzania tunatimiza miaka 60 ya Uhuru wetu
| na hivyo nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Uhuru Kenya
| awe mgeni rasmi katika maadhimisho yale ya miaka 60 ya Uhuru wetu
| kwahiyo hayo ndiyo ambayo mpaka sasa hivi tumezungumza na kakangu
| na kweli nataka niseme
| mimi na ujumbe wangu tunajihisi tuko nyumbani
[ahsante]
| ahsateni sana
| ahsante sana

  1. 原话为tusitakwenda []
 

ynshen