Uhuru na pendo

Iwe siku ya bukheri, abee ywakuita ng’o
Pamoja na neno duni, kusifu kwa mdukuo
Mengi hadhi pia hasi, si kimio ‘la kiuno
Niseme wazi yanavyo, dogo la wema halipo!

Toka ghuba ziwa kuu, jamadari na dalali
Waleta pao uhuru, hawataki pingamizi
Ningenena ipo siku, ama kunyamaza ‘ngali
Niseme wazi yanavyo, dogo la wema halipo!

Hata mzaha wapendwa, wanijia kwa mafungu
Mfano wa mambo haya, kweli kupora hatamu
Hapewi ada mfiwa, mwashangilia shauku
Niseme wazi yanavyo, dogo la wema halipo!

Licha kinyesi na choyo, bado jina ngojera
Awe chembe cha moto, na kijimo kipe sura
Ngamani marejeo, kama neno geni tomba
Niseme wazi yanavyo, dogo la wema halipo!

yns
2021.05.15

 

[Makavazi] Mahojiano ya Hussein Issa Tuwa, rais wa UWARIDI, na ITV, Tanzania, mwaka mpya wa 2021

https://www.facebook.com/187353645175928/videos/410301496947059

下载:HusseinIssaTuwa&ITV

[KUNAKILI KUANZIA 00:53]

Moderater (baadae kwa kifupisho cha M): Hussein Tuwa karibu sana hapa ITV. Hapa inaonyesha kwamba wewe ni Rais wa UWARIDI. UWARIDI kwa maana ya nini? UWARIDI ni kitu gani?

Hussein (baadae kwa kifupisho cha H): Mimi ni urais wa UWARIDI ambao ni umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira Tanzania.

M: Umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira?

H: Unajua UWARIDI kuna waandishi wa riwaya halafu kuna waandishi wa riwaya wenye dira kuna tofauti yale. Sasa sisi kwenye UWARIDI tumejipambanua kwamba tunafanya uandishi wa riwaya lakini kwa malengo mahsusi ya kuisogeza kwanza fasihi ya Tanzania mbele, kuiweka juu ionekane lakini vile vile nasisi waandishi wenyewe tuweze kunufaika kwa kazi za mikono yetu kwahiyo tunavofanya vitu tunakwenda kwa malengo tunakuwa tuna dira maalum ya kutuongoza. siyo tunaandika, kwa waandishi miongoni mwa waandishi tu hapana ni waandishi wenye dira tunaandika kwa malengo, tunaandika kwa ueledi, tunaandika kwa kufuata maadili, tunaandika kwa kuwa na utaratibu mahsusi ambao tunaamini tukifuata ule utaratibu tutafika kule tutakapofika, au tutafikisha fasihi ya Tanzania kule inapopaswa iwe.

…